Jumamosi 12 Julai 2025 - 13:00
Radi amali ya Al-Azhar kuhusu safari ya “Maimamu wa jamaa katika misikiti ya Ulaya” kwenda Israel

Hawza/ Al-Azhar ya Misri imelitaja kundi la watu waliokwenda hivi karibuni Israel na kujieleza kuwa “Maimamu wa jamaa katika misikiti ya Ulaya” kuwa ni “kundi lililopotoka,” na kuilaani vikali safari hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tajuma cha  Shirika la Habari la Hawza, Al-Azhar ya Misri imelaani vikali safari ya hivi karibuni ya watu waliodai kuwa wao ni “maimamu wa misikiti ya Ulaya” kwenda Israel, na imewataja washiriki wa safari hiyo kuwa ni “kundi lililopotoka ambalo si wawakilishi wa Uislamu wala Waislamu.”

Jumatatu iliyopita, ofisi ya Isaac Herzog, rais wa Israel, katika taarifa yake ilitangaza kuwa alipokea katika ofisi yake iliyopo Yerusalemu Magharibi “maimamu wa misikiti na viongozi wa jamii ya Kiislamu kutoka Ufaransa, Ubelgiji, Uholanzi, Italia na Uingereza.”

Herzog alidai kuwa ujumbe huo, ulioongozwa na Hassan Chalghoumi, ulikuwa na nyuso mashuhuri za Kiislamu waliokuja Israel kwa lengo la kuwasilisha ujumbe wa amani, kuishi kwa pamoja, na ushirikiano kati ya Waislamu na Wayahudi, na kati ya Israel na ulimwengu wa Kiislamu.

Al-Azhar, katika kauli yake kuhusu safari hiyo, ilisema:

“Kwa masikitiko makubwa tunaifuatilia safari ya baadhi ya maimamu wa misikiti wa Ulaya waliodai kuwa ni wawakilishi wa Uislamu, wakiongozwa na mtu anayeitwa Hassan Chalghoumi, waliokwenda katika ardhi zilizokaliwa kwa mabavu za Palestina na kukutana na rais wa utawala wa Kizayuni unaoikalia ardhi hiyo kwa nguvu, na matamshi yao yenye mashaka na yenye nia mbaya kwamba safari hiyo imelenga kuimarisha maelewano na mazungumzo baina ya dini mbalimbali.”

Al-Azhar, katika taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wake wa Facebook, ilieleza kuwa maimamu hao wa jamaa kwa madai ya ziara hiyo, wameyafumbia macho mateso wanayoyapitia watu wa Palestina yanayosababishwa na mauaji ya halaiki, uvamizi wa kihistoria, mauaji ya umati, na kuendelea kuuawa kwa watu wasio na hatia kwa zaidi ya miezi 20 mfululizo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha